Bondia Gennady Golovkin ameonyesha kweli yeye ni
hatari na hapigiki baada ya kumtwanga kwa KO Willie Monroe mwenye asili ya
Cuba.
Monroe alionekana ni bondia mbishi zaidi lakini
alishindwa kuvumilia makonde ya Golovkin raia wa Khazakstan na kukaa chini
katika raundi ya sita.
Kwa ushindi huo Golovkin anakuwa amecheza
mapambano 33 bila ya kupoteza hata moja.
Kitu kizuri zaidi katika ubora wake ni kwamba Golovkin
ameshinda KO 30 katika mechi zake 33. Hii ni hatari, cheki mapicha.
0 COMMENTS:
Post a Comment