HANS POPPE
Simba wameendelea kusisitiza kuwa wanasubiri jibu la mwisho la Kocha Goran Kopunovic kuhusiana uamuzi wake.
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema, iwapo Kopunovic atakaa kimya, basi watajua amesema hapana.
"Nilishasema kwamba tunasubiri Ijumaa (kesho) atoe jibu. Akikaa kimya tutajua ni hapana na mara moja tutaanza kazi ya kusaka kocha.
KOPUNOVIC |
"Kwa fedha anazotaka yeye tumemueleza wazi Simba haiwezi kulipa hata kidogo," alisema.
Imeelezwa Kopunovic ambaye sasa yuko kwake nchini Hungary kwa mapumziko ametaka alipwe mshahara wa zaidi ya dola 10,000 kutoka dola 5,000 alizokuwa akilipwa awali.
Pia ameutaka uongozi wa Simba kumpa dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 100 kama ada ya usajili. Jambo ambalo Simba wamemuweka wazi kwamba hawawezi kufanya hivyo.
Simba imemaliza katika nafasi ya tatu ikiwa chini ya Kopunovic. Licha ya kuonyesha kiwango kizuri, bado imekosa nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa kwa msimu wa tatu mfululizo.
Hata hivyo, Hans Poppe amesisitiza bado wana nafasi ya kufanya vema msimu ujao kwa kuwa wachezaji wengi vijana katika kikosi chao watakuwa wamezidi kuimarika.
0 COMMENTS:
Post a Comment