Timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la
Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters Rest - Protea iliyoypo pembeni
kidogo ya jiji.
Taifa Stars ambayo iliondoka
jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam na kufika OR Tambo saa 5
usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja
na Watanzania wanaoishi jijini humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.
Safari ya kutoka Johannesburg
kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa mawili na msafara wa Taifa Stars
unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.
Wachezaji waliopo na timu
Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar
Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma,
Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma
Luizio, John Bocco, Mrisho Ngasa na Simon Msuva.
Kikosi cha Taifa Stars
kinatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Rustenburg Impala
Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa
11 jioni kwa Afrika Mashariki.
0 COMMENTS:
Post a Comment