Mshambuliaji wa
Barcelona, Lionel Messi ni hatari aisee. Pamoja na ugumu wa Atletico Madrid
amepiga bonge la bao na kuibeba timu yake.
Ushindi huo wa
bao 1-0 umeipa Barcelona uhakika wa kuwa bingwa wa La Liga baada ya kufikisha
pointi 93.
Real Madrid
yenye pointi 89 baada ya ushindi wa jana, itafikisha 92 kama itashinda mechi ya
mwisho.
Barcelona nayo
ina mchezo mmoja mkononi. Ambao sasa unabaki kuwa kama mechi ya kirafiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment