May 12, 2015

Kocha wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet amezindua rasmi kitabu chake kinachohusiana na kazi yake ya ukocha katika nchi mbalimbali za Afrika.


Baadhi ya nchi alizozizungumzia ni Afrika Kusini na Tanzania ambayo alifanya kazi akiwa Yanga.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji aliinoa Yanga na kuisaidia kuipa ubingwa wa Kagame kabla ya kitibuana na uongozi na baadaye nafasi yake kuchukua Ernie Brandts raia wa Uholanzi.
Kitabu hicho cha Saintfiet kimeanza kuuzwa katika nchi Ubelgiji pamoja na Uholanzi.
Baadhi ya picha ni zile zinazoonyesha akiwa bungeni na kikosi kizima cha Yanga na uongozi wa timu hiyo pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Pia picha ambayo amelibeba Kombe la Kagame akiwa pamoja na nahodha wa Yanga, Nadir Haoroub 'Cannavaro' na Rais wa Rwanda, Paul Kagame walipokwenda kumtembelea katika Ikulu ya Rwanda.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic