NGASSA AKIWA NA KOCHA PHIRI AMBAYE ALIMPOKEA BAADA YA KUTUA AFRIKA KUSINI. |
Mrisho Ngassa ametua zake
Free State Star ya Afrika Kusini na kupokelewa kwa shangwe.
Mmoja wa waliompokea ndani
ya aneo la Bethlehem ni Kocha Kina Phiri, mshambuliaji wa zamani nyota wa
Malawi.
Ngassa amejiunga na Free
State Star akitokea Yanga ambayo ameichezea kwa mafanikio makubwa.
Ngassa ameiambia SALEHJEMBE
kutoka Afrika Kusini kuwa mambo yanakwenda vizuri.
“Lakini ningependa nimalize
mambo kadhaa muhimu hapa halafu tutazungumza,” alisema mtoto huyo wa
mshambuliaji nyota wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba, Khalfan Ngassa.
0 COMMENTS:
Post a Comment