May 12, 2015

Kocha Goran Kopunovic amesema ni kweli hajaridhishwa na viwango vya wachezaji watatu Waganda.


Kopunovic raia wa Serbia amesema zaidi amefurahishwa na Emmanuel Okwi na Juuko Murishid, waliobaki, haoni kama wanamfaa. Lakini haoni sababu ya kufikicha kwa Waganda, Simon na Dan Sserunkuma pamoja na Joseph Owino.

Amesisitiza hawakuonyesha kiwango cha kumvutia ambacho anaona kuwa uwepo wao ulikuwa msaada Simba.

Akizungumza na SALEHJEMBE, leo. Kopunovic amesema, hana sababu ya kuficha.

“Bado sijawa na uhakika kama nitabaki Simba au la. Lakini ukweli ndiyo huo sijafurahishwa na viwango vyao wote watatu.

“Angalau kidogo Owino, lakini mkataba wake umekwisha kama ilivyo kwangu. Uongozi unaweza kujua utafanya nini.

“Nisingependa kuzungumzia mengi zaidi kwa kuwa hata mimi nimemaliza mkataba wangu,” alisema Kopunovic.
Kocha huyo tayari yuko uwanja wa ndege na anatarajia kuondoka leo kurejea kwao.


Kopunovic raia wa Serbia anarejea nchini Hungary ambako ndiyo yalipo makazi yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic