ADEBAYOR AKIWA NA ROTIMI... |
Emmanuel Adebayor ameendelea
kuibua madudu ya ndugu zake baada ya kusema mdogo wake aliiba jezi zake mbili
alizokuwa amepewa na nyota wakubwa duniani.
Adrbayor amesema mdogo wake
wa mwisho aitwaye Rotimi aliiba jezi mbili alizopewa na Marc-Vivien Foe na gwiji
wa Real Madrid, Zinedine Zidane.
Pia Rotimi alishirikiana na
rafiki zake kuiba mkufu wenye thamani ya pauni 25,000 aliomnunulia mama yake.
Kijana huyo, ndiyo yule
aliyemuelezea mwanzo kwamba aliiba simu za wachezaji 21 alipomlipia kwenye
akademi apate mafunzo nchini Ufaransa.
Adebayor amekuwa akitema ‘nyongo’
kuhusiana na ndugu zake ambao awali walianzisha kumlaumu.
Aidha, alisimulia kuwa
mdogo wake huyo pia aliiba vifaa mbalimbali kwa wenzake ikiwamo kutoka kwa
mtoto wa nyota wa zamani wa Cameroon, Jack Song’oo na kusababisha uhusiano wake
na familia ya mchezaji huyo kuzorota.
0 COMMENTS:
Post a Comment