Kocha Goran Kopunovic
amethibitisha kwamba keshi ndiyo siku atakayotoa jibu kuhusiana na ofa
aliyopewa na Simba.
Akizungumza moja kwa
moja Budapest, Hungary, leo Kopunovic amesema atawaambia Simba kama amekubali au
la.
“Ni kweli tulikubaliana
Ijumaa, si mbali ni kesho. Nitawaeleza nini kinaendelea na nimeamua vipi.
“Ningependa kubaki
Simba, lakini kumbuka mimi pia ni binadamu nina mahitaji muhimu,” alisema.
Leo mchana, Mwenyekiti
wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema wanasubiri jibu la
kocha huyo kesho.
Kama atakuwa tayari
sawa, asipokuwa tayari nao watamuacha na kuendelea kusaka kocha mwingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment