Kuna taarifa waamuzi watatu
waliochezesha mechi kati ya Stand United dhidi ya Ruvu Shooting wamefungiwa
miezi 12.
Mwamuzi wa kati siku hiyo
alikuwa ni Amon Paul kutoka Mara.
Taarifa za waamuzi hao
kufungiwa miezi 12 tayari zimezagaa kwenye vyombo vya habari.
Hata hivyo kumekuwa kumekuwa na
ugumu wa Maofisa wa Bodi ya Ligi Kuu akiwemo Kaimu Mtendaji Mkuu, Fatuma
Abdallah akionekana kutotaka kuthibitisha au kukataa.
“Taarifa zikiwa rasmi
nitawataarifu, kwa sasa bado hatujazungumza kuhusiana na hilo,” alisema.
Stand ilishinda kwa bao 1-0 na
kuididimiza Ruvu Shooting ambayo imeteremka hadi daraja la kwanza.
Hali hiyo ilifanya Ruvu
Shooting kukata rufaa na jana kikao cha kusikiliza rufaa hiyo na nyingine
kilikaa. Hakikumaliza kimekaa tena leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment