Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema watafanya kila juhudi kumbakiza kiungo Haruna Niyonzima na wengine wanaohitajika.
"Lakini tutakuwa makini sana katika suala la usajili kwa kuwa tunajua umuhimu wake," alisema Dk Tiboroha.
"Kikubwa wanapaswa kutuamini na kama suala litakuwa limekamilika, basi tutawataarifu.
"Tunajua umuhimu wa Niyonzima na baadhi ya wachezaji wengine ambao wanatakiwa kubaki na tunaendelea kulishughulikia hilo."
Kuanzia jana jioni kwenye mitandao mbalimbali, zilizagaa taarifa kwa tayari Yanga imeongeza mkataba na kiungo huyo Mnyarwanda.
Lakini leo asubuhi, uongozi wa Yanga ulikanusha taarifa hizo, hali kadhalika Niyonzima mwenyewe alisema hajasaini mkataba wowote akizikataa taarifa hizo za mitandaoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment