Uongozi wa Ndanda FC ya Mkoa wa Mtwara, umeeleza kuwa unadaiwa na
wachezaji wake kiasi cha shilingi milioni 10 ikiwa ni fedha za usajili na
mishahara ya mwezi mmoja.
Ndanda ambayo ilipanda daraja msimu uliyopita, ilinusurika kushuka
daraja kutokana na kushika nafasi za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Katibu wa Ndanda, Suleiman Kachele, amefunguka kuwa wanawashukuru
wachezaji wao kutokana na kuibakiza timu katika ligi na kudai wanachosumbuka
nacho kwa sasa ni deni hilo.
“Tunawashukuru wachezaji wetu kuibakiza timu katika ligi lakini
tunajua kuwa wanatudai, tupo katika mchakato wa kuhakikisha tunazipata fedha
hizo ili tuweze kuwalipa,” alisema Kachele.
0 COMMENTS:
Post a Comment