KOCHA MKUU WA TOTO AFRICAN, JOHN TEGETE AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA TOTO AFRICAN |
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amewaonya
viongozi wa Toto Africans ya Mwanza iliyopanda kucheza Ligi Kuu Bara kutokana
na migogoro inayoendelea katika timu hiyo.
Toto imekuwa katika misigano tangu kupanda daraja ambapo tayari
viongozi mbalimbali wameachia ngazi akiwemo mwenyekiti wa timu hiyo, Omary
Mbalamwezi, mweka hazina, Geofrey Kyabula, pamoja na mwanasheria wake, Gasper
Mwanalyela.
Akizungumzia sakata hilo, Malinzi alisema amepata taarifa za timu
hiyo ya jijini Mwanza kuwa na malumbano huku akiwataka kukaa chini mapema,
vinginevyo hawatadumu katika ligi kuu.
“Nimesikia taarifa za migogoro ya Toto na imenishangaza sana kwa
timu ambayo imepanda daraja, badala ya kufanya usajili wao wanaendekeza migogoro,
hili si jambo zuri, wasipoamka mapema watashuka daraja msimu ujao.
“Nimesikia kuwa wanagombana kwa sababu ligi kuu kuna fedha za
udhamini. Ninawataka wakae chini na kuangalia namna nzuri ya kutatua matatizo
yao, wasiutie aibu Mkoa wa Mwanza,” alisema Malinzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment