Kocha Carlo Ancelotti wa Real Madrid amesema kama
uongozi wa timu hiy utamtimua, basi kitu cha kwanza atakachofanywa ni kwenda
kufanyiwa upasuaji wa mgongo.
Ancelotti amesema akifanyiwa upasuaji huo atalazimika
kupumzika kwa mwaka mzima ili kuhakikisha anapona kabisa.
Bado kumekuwa hakuna uhakika kama Muitaliano huyo
atabaki na Madrid baada ya kushindwa kubeba hata kombe moja msimu huu.
Taarifa zimeeleza amekuwa na mpango wa kurejea AC
Milan kama Madrid watamtupia virago vyake.
0 COMMENTS:
Post a Comment