RAGE AKIWA NA HASSAN DALALI NA GEOFREY NYANGE 'KABURU'. |
Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba na mbunge wa sasa wa Tabora
Mjini, Ismail Aden Rage, amesema timu za Yanga na Azam FC zimepata nafasi mbili
za juu katika Ligi Kuu Bara kwa kuwa zilipendelewa na waamuzi katika michezo
yao.
Akizungumza mjini Dodoma ambapo anahudhuria vikao vya bunge, Rage
alisema waamuzi ndiyo wamechangia Yanga kuwa bingwa kisha Azam kushika nafasi
ya pili.
“Sina ushahidi wa moja kwa moja kwamba hawa mabwana walikuwa
wanapendelewa ila naomba nieleweke kuwa marefa wamechangia sana Yeboyebo
(Yanga) kuchukua ubingwa hata Azam nao hivyohivyo.
“Katika mzunguko wa kwanza timu zao zilikuwa hazifanyi vizuri lakini
katika mzunguko wa pili baada ya kuona hali inakuwa ngumu ikapidi sasa waanze
kutumia mambo yetu ili kuhakikisha ushindi unapatikana,” alisema Rage.
Kuhusu Simba alisema: “Timu ina wachezaji wazuri ambao wanahitaji
kukaa pamoja muda mrefu ili wazoeane. Unajua Mwarabu dawa yake ni Simba tu hawa
Yanga wataendelea kuumizwa tu.”
Rage aliongeza kuwa, ni vema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
likaongeza posho kwa waamuzi kwa kuwa umuhimu wao ni mkubwa katika soka.
0 COMMENTS:
Post a Comment