Kocha wa zamani wa Yanga, Marcio Maximo na aliyekuwa msaidizi wake
klabuni hapo, Leonardo Neiva, wamefurahishwa na timu yao hiyo kutwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara hata kabla ya msimu kumalizika.
Makocha hao ambao ndiyo waliokuwa wakiifundisha timu hiyo mwanzoni
mwa msimu huu, wametuma salamu za pongezi kwa viongozi, wachezaji na mashabiki
wa klabu hiyo.
Akizungumza kutoka Brazil, Neiva ambaye kwa sasa anainoa timu
ya Prudentopolis ya Brazil, alisema yeye na Maximo wamezipokea taarifa hizo kwa
furaha na kwa pamoja wanaipongeza Yanga kwa hatua hiyo.
“Nimefurahi kusikia Yanga ndiyo mabingwa wa ligi, sikuweza kuficha
furaha yangu, Maximo naye amezipata taarifa hizo, amefurahi pia.
“Kwa pamoja tunawapongeza wachezaji waliopambana hadi kufikia hapo
bila kuwasahau viongozi na wote waliofanikisha hilo,” alisema Neiva ambaye yeye
na Maximo walifukuzwa Desemba, mwaka jana baada ya kufungwa na Simba katika
mechi ya Nani Mtani Jembe.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment