Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema
bado wana matumaini ya kupambana na kufanya vema dhidi ya Etoile du Sahel.
Pluijm ambaye yuko mjini Sousse, Tunisia na
kikosi cha Yanga kwa ajili ya kuivaa Etoile du Sahel amesema matumaini ni
makubwa lakini lazima wapambane.
“Tunajua tokea mwanzo haitakuwa kazi lahisi,
lakini tuna matumaini ya kufanya vema. Ila lazima tupambane kweli kwa kuwa wana
kikosi kizuri,” alisema.
Wachezaji wa Yanga wameonekana kuwa na
morali na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Leo asubuhi wachezaji hao pamoja na benchi
la ufundi na viongozi, wamepata kifungua kinywa pamoja.
Mechi itaoneshwa na kituo gani
ReplyDelete