Timu ya Simba imeshindwa kuipata saini ya kiungo mshambuliaji wa
timu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya kushindwa kutoa dau la shilingi
milioni 50.
Mkataba wa Singano umemalizika hivi karibuni mara baada ya
kumalizika kwa msimu wa 2014/15 na inavyoonekana hali ni ngumu kwa kuwa klabu
hiyo imeshindwa kumshawishi kusaini mkataba mpya.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo kimesema kuwa
Singano amegoma kusaini kwa dau la shilingi milioni 30 mkataba wa miaka miwili.
“Dili la Messi la kusaini mkataba mwingine wa kuichezea Simba
limeshindikana, baada ya pande zote mbili kwa maana ya mchezaji na viongozi
kushindwa kufikia muafaka.
“Alitaka milioni 50, viongozi walitaka kumpa milioni 30, sawa na dau
la (Said) Ndemla, yeye akalikataa. Yote hayo yanatokana na usajili wa Mkude
(Jonas) ambaye alipewa shilingi milioni 60 na gari la kutembelea Toyota Mark 11
Grande, hivyo wachezaji wengine nao wanataka kiasi kikubwa cha fedha wakiamini
watapata,” kilisema chanzo hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment