May 10, 2015


Uongozi wa Simba, unasubiri ripoti ya Kocha Goran Kopunovic ili kuanza mchakato wa usajili.


Simba wameamua kuusubiri ripoti hiyo ili kupata uhakika wa nini kinachotakiwa kufanya mabadiliko.

Kikosi cha Kopunovic raia wa Serbia kimemaliza kikiwa katika nafasi ya tatu.

Nafasi hiyo inaifanya Simba kupoteza nafasi ya kushiriki tena katika michuano ya kimataifa.

“Baada ya ripoti ya Kopunovic, basi ataikabidhi ripoti kwa uongozi na mchakato utaanza,” alisema Haji Manara, msemaji wa Simba.


Simba imepania kufanya mabadiliko katika kikosi chake ili kujihakikishia kubeba ubingwa ambao imeukosa kwa misimu mitatu sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic