Yanga ina mpango wa kusajili beki wa kati kwa ajili ya kusaidiana na Kelvin Yondani na Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Uamuzi huo wa Yanga unatokana na kuona Yondani na Cannavaro kuwa wakiwa majeruhi difensi inayumba.
"Kweli tunahitaji beki wa kati tena mzoefu ambaye atasaidiana na Cannavaro na Yondani," alisema Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm.
"Mara kadhaa tumekuwa tukimtumia Twite kwa kuwa hatuna beki wa kati mwenye uzoefu. Kumbuka tunakwenda katika michuano ya kimataifa.
"Mchakato umeanza na tunataka kufanya mambo ya uhakika katika hili."
Pia Yanga inataka kuongeza mshambuliaji ambaye ataongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment