Kamati ya Usajili ya Simba, imepanga kumpandisha beki mmoja wa kati kutoka kikosi cha vijana.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zacharia Hans Poppe amesema pamoja na kuendelea kutafuta beki wa kati, watampandisha kijana mmoja.
"Simba imekuwa na kawaida ya kukuza vijana, huu ni utamaduni wetu ambao nafikiri ndiyo umekuwa ukisaidia kukuzwa kwa vijana wengi sana.
"Tutampandisha beki mmoja wa kati kutoka katika kikosi cha vijana lakini pia tutasajiri mabeki wengine wa kati kwa ajili ya kujiimarisha," alisema Hans Poppe.
Tayari Simba imeishamtema beki mkongwe Mganda, Joseph Owino na sasa imebaki na mabekiw awili ambao ni Hassan Isihaka na Mganda, Juuko Murishid.
0 COMMENTS:
Post a Comment