![]() |
| MSUVA AKIWA KWENYE UWANJA WA SOCCER CITY JIJINI JOHANNESBURG, JANA. |
Kiungo Simon Msuva
anatarajia kuanza majaribio katika kikosi cha Bidvest Wits leo.
Timu hiyo maarufu kwa
mashabiki kama Wits inashika nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Mmoja wa marafiki wa Msuva
aliyeko jijini Johannesburg amesema kiungo huyo atafanya majaribio kwa siku
tatu.
“Wamesema hadi Jumamosi,
baada ya hapo ataanza safari ya kurejea Tanzania.
“Yuko hapa, amefika salama
na tulikuwa naye uwanjani wakati Wits ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya wakongwe
Kaizer Chiefs jana,” alisema.
Timu hiyo inamilikiwa na Chuo Kikuu kikongwe barani Afrika cha Bidvest kilicho katikati ya jijini la Johannesburg.








0 COMMENTS:
Post a Comment