Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally, ametangaza kujiuzulu nafasi
hiyo.
Stephene aliingia madarakani mwaka jana mara baada ya uongozi
kuingia madarakani kuiongoza timu hiyo chini ya Rais Evans Aveva.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Stephene amesema kikubwa
kilichomfanya ajiuzulu ni kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo.
Katibu huyo alisema madaktari wa Hospitali ya Muhimbili ya jijini
Dar es Salaam ndiyo waliomshauri apumzike kwa muda usiojulikana kutokana na
ugonjwa unaomsumbua baada ya kufanyiwa vipimo.
“Cha kwanza kabisa katika mwili wa binadamu ni afya na hayo mengine
yanakuja baadaye, madaktari wamenishauri nipumzike kufanya kazi kwa muda
usiojulikana kwa ajili ya kujiuguza kwanza. Ugonjwa sitaweza kuutaja kwa sasa,
tayari nimekabidhi barua kwa uongozi.
“Ninaomba nichukue muda huu kuwashukuru viongozi, wachezaji na
mashabiki kwa jumla kwa kipindi chote nilichokuwa ninaiongoza Simba,” alisema
Stephene.
0 COMMENTS:
Post a Comment