June 17, 2015

BAHANUZI WAKATI AKIITUMIKIA YANGA.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Said Bahanuzi, amesema kuwa anatarajia kuifikisha mbele ya vyombo vya sheria klabu yake hiyo kufuatia kukatishwa mkataba wake bila ya kulipwa kitu chochote.


Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuchukua tuzo ya mfungaji bora ya michuano ya Kombe la Kagame mwaka 2012, akiwa na Yanga, mambo  yalikuwa si mambo kufuatia kutopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, amesema kuwa ataifikisha mahakamani klabu yake hiyo iwapo haitajibu barua yake.

Bahanuzi ni miongoni mwa wachezaji saba waliotupiwa virago vyao Yanga pamoja na Omega Seme, Thabiti Abdul, Anthony Matogolo, Danny Mrwanda, Jerryson Tegete  ambao bado hawajamaliza mikataba yao pamoja na Nizar Khalfan ambaye mkataba wake uliisha.

Bahanuzi ambaye aliichezea Polisi Moro kwa mkopo msimu uliyopita, alisema kuna mwanasheria ambaye anafanyanaye mazungumzo na kuupitia upya mkataba wake ili kuweza kujua nini kimejiri kisha kuandika barua na kuiwasilisha Yanga ili kuweza kupata majibu juu ya malipo yake.
 “Nimepata barua ya kuachwa na Yanga Mei 21 ambayo inaonyesha kuwa wamevunja mkataba na hawatahusika juu ya kunitafutia timu nyingine kwa ajili ya kuichezea msimu ujao, jambo hilo limenifanya kutopata timu hadi sasa kwa kuwa ilikuwa kama siri, hawakutangaza kama ilivyo kawaida, hakuna timu inayojua kama nipo huru.

“Leo (Jumatatu), natarajia kukutana na mwanasheria wangu hapa nyumbani kwa ajili ya kuupitia upya mkataba kisha kuangalia dosari ili kuweza kujua nini kimetokea kisha tutawaandika barua kwa ajili ya kuipelekea klabu ambapo tutaisubiria ndani ya siku kumi hadi 15 kupata majibu.

“Na iwapo hawatatujibu ndani ya siku hizo, itabidi nilifikishe mbele ya sheria suala hili ili niweze kulipwa haki zangu kwa kuwa wao ndiyo wamevunja mkataba na mimi,” alisema Bahanuzi.


Kuhusiana na suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alisema: “Hatutahusika na suala la kuwatafutia timu wachezaji hao kwa kuwa kuna kipengele fulani ambacho kipo ndani ya mikataba yao, ambacho kinaeleza kuwa  iwapo hatacheza katika kiwango tulichokubaliana tunaachana naye, hivyo hatutahusika na kuwatafutia timu nyingine wachezaji tuliowaacha.”

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Alitakiwa kujua amekutana na wasomi, muda wa kubweteka na kusubiria mishahara ya bure huku hujitumi umekwisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic