June 19, 2015


Kiungo wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, jana Alhamisi alianza mazoezi kwa mkwara mzito kwa kufanya mambo kadhaa yaliyoonyesha kweli amejipanga na safari hii anataka kufanya kweli.


Kwanza Coutinho ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza kuwasili uwanjani huku akimfunga bao la kiwango cha dunia kipa, Ally Mustapha ‘Barthez’.

Coutinho, sambamba na mshambuliaji wa timu hiyo, Kpah Sherman, raia wa Liberia, wamekuwa wachezaji wa kwanza wa kimataifa kuripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar chini ya kocha Hans van Der Pluijm na msaidizi wake, Boniface Mkwasa ‘Master’.

Coutinho aliingia uwanjani akiongozana na Sherman, ambapo waliwasalimia wenzao wa benchi la ufundi, wakarejea kwenye gari kuchukua viatu na kuanza mazoezi huku wachezaji wenzao wakiendelea kupiga soga, kitendo kilichomkera Pluijm mpaka walipoitwa na Mkwasa kwa ajili ya kuanza mazoezi.

Katika mazoezi hayo, wawili hao walipewa programu maalum ya mazoezi ambapo walianza kwa kutembea na baadaye kukimbia kabla ya kujiunga na wenzao kwa mazoezi ya pamoja.

Mbali na hapo, Coutinho alimtesa Barthez kwa kufunga bao zuri baada ya kutishia kama anapiga shuti kisha ‘akauchop’ mpira ambao ulitinga wavuni huku kipa huyo akiwa hoi akishindwa kuamini kilichofanywa na Mbrazili huyo.

Mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo wakawa wanampigia makofi na kumshangilia mara kadhaa kutokana na kuonyesha kujituma, lakini upande wa Pluijm, akimzungumzia mchezaji huyo, alisema:

“Nimefurahishwa na kiwango cha Coutinho, anaonekana anajituma lakini kuna baadhi ya vitu lazima avifanyie kazi ikiwemo kukaba akiwa uwanjani. Hilo ni tatizo ambalo amekuwa nalo siku nyingi, anasaidia mashambulizi lakini hawezi kukaba.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic