Yanga jana imepata ushindi
wake wa kwanza kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara kwa kuifunga Friends
Rangers mabao 3-2 huku mshambuliaji mpya, Malimi Busungu akipiga mbili pekee.
Mechi hiyo, ilipigwa
kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam iliyoudhuliwa na watazamaji wengi
waliofika kuwaangalia nyota wapya waliowasajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi
kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo, Kocha Mkuu
wa Yanga aliwaanzisha wachezaji watatu pekee wa kikosi cha kwanza
ambao ni Kelvin Yondani, Salum Telela na Juma Abdul huku wengine wakiwa wapya
waliosajili kwa ajili ya msimu ujao na wa kikosi cha pili.
Wachezaji wapya
aliowaanzisha katika mechi hiyo kwa hiyo kuangalia uwezo wao ni Deus Kaseke,
Benedicto Tinoco na Lansana Kamara.
Katika mechi hiyo, Yanga
ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza kupitia kwa Mliberia, Kpah
Sherman akiunganisha pasi safi ya Busungu katika dakika 20 ya mchezo huo.
Bao hilo alikudumu muda
mrefu baada ya mshambuliaji wa Friends Rangers, Ally Rooney kupiga faulo safi
nje ya 18 na kumchambua Tinoco baada ya Kelvin Yondani kumchezea vibaya.
Yanga ilipata bao la pili
kupitia kwa Busungu baada ya kugongeana na Sherman kabla ya kumchambua kipa wa
Friends Rangers, bao hilo alikudumu baada ya wapinzani kusawazisha kupitia kwa
Cosmas Lewis ‘Baloteli’ kwa shuti kali la mita 20 lililomshinda Ally Mustapha
‘Barthez.
Katika dakika ya 87,
Busungu akaifungia bao la tatu Yanga akiunganisha krosi safi ya kiungo
mshambuliaji Mbrazili, Andrey Coutinho na kufanya mechi hiyo kumalizika kwa
Yanga kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment