June 24, 2015


Benchi jipya la Taifa Stars likiongozwa na mshauri wake wa ufundi, Abdallah Kibadeni litakutana na wachezaji wa kikosi cha Taifa Stars, keshokutwa.


Kibadeni ni mmoja wa magwiji wa soka nchini, aliwahi kuwika akiwa na Majimaji, Simba na Taifa Stars.

Mkutano huo kati ya Kibadeni, Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa , msaidizi wake Ahmed Morocco watakutana na wachezaji hao katika hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kujadili suala la uzalendo.

Mkwasa amesema watafanya hivyo kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji lakini pia kuwapa wachezaji somo la uzalendo.

Tayari Mkwasa ametangaza kikosi chake huku Manyika Peter, kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars akiwapewa kazi ya kuwanoa makipa.

Kikosi kipya:
Mwadini Ally-Azam
Ally Mustapha-Yanga
Mudathir Khamis-KMKM
Shomari Kapombe-Azam
Michael Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed Hussein-Simba
Mwinyi Hajj-KMKM
Nadir Haroub-Yanga
Kelvin Yondani-Yanga
Aggrey Morris-Azam
Hassan Isihaka-Simba
Jonas Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon Msuva-Yanga
Said Ndemla-Simba
Ramadhan Singano-Simba
Salum Telela-Yanga
Frank Domayo-Azam
Atupele Green-Kagera Sugar
Rashid Mandawa-Mwadui
Ame Ally-Azam
Deus Kaseke-Yanga
Samuel Kamuntu-JKT



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic