KATIKA
jambo ambalo limekuwa likipasua kichwa changu kwa wiki hizi mbili bila haa ya
kupata jibu, ni hili linalomhusu kiungo wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’.
Messi
na klabu yake ya Simba, wamekuwa katika malumbano yasiyoisha huku kila upande
ukisema uko sahihi kuhusiana na mkataba.
Messi
anasema mkataba wake unaisha mwaka huu kwa kuwa ulikuwa ni wa miaka miwili,
Simba wanasema unakwisha mwakani kwa kuwa ulikuwa ni wa miaka mitatu.
Simba
wana uhakika kwa kuwa wana uthibitisho, Messi naye ana uhakika kwa kuwa ana
mkataba wake mkononi. Kila mmoja anashikilia msimamo wake kuhusiana na uhakika
wa upande wake.
Lakini
kumeanza kuonekana walakini kidogo kwa upande wa mkataba wa Messi, kwamba kweli
unaonyesha ni miaka miwili, lakini ni kopi, si ule orijino. Jambo ambalo
linawafanya Simba watumie nafasi hiyo kuhoji.
Bado
Messi hajatoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na ukweli wa hilo. Kwamba kama
kweli ana mkataba orijino, ingawa nilisikia alisema huo ndiyo aliopewa!
Kawaida
mikataba inakuwa hivi, wachezaji wanapoingia mkataba na klabu, wanasaini mara
tatu kama ilivyo kwa ofisa upande wa klabu. Baada ya hapo unafanyika mgawo mara
tatu.
Mgawo
unakuwa hivi; klabu, mchezaji na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kama ni
makubaliano, kunaweza kuwa na kopi maalum kwa ajili ya mwanasheria. Sasa vipi
Messi leo ana kopi na si orojino?
Hapa
ndipo maswali mengi nimejiuliza bila ya majibu. Kwamba alipewa akaupoteza? Au
ameamua tu kuuchakachua?
Pia
najiuliza au Simba hawakumpa makusudi wakati anasaini? Kama hivyo ndiyo
ilivyokuwa, wao wanafaidika na nini sasa? Kwa kweli kunakuwa na maswali mengi
sana.
Messi
ni kati ya vijana wenye nidhamu kabisa, ninamfahamu kama wadogo zangu ndiyo
maana nimekuwa nina hofu kubwa kwamba amechakachua. Lazima kutakuwa na tatizo
katika mkataba wa viongozi wa Simba waliomsainisha, au umakini sehemu fulani.
Najaribu
kujiuliza pia, yule meneja wake ambaye tumekuwa tukimsikia akizungumza kwenye
vyombo vya habari, vipi alishindwa kumsimamia wakati wa kusaini mkataba. Narudi
tena kuangalia, huyo meneja kama alimsimamia, vipi alishindwa kujua umuhimu wa
mkataba orijino?
Naanza
kuwaza, nikipewa nafasi ya kutangaza adui au tatizo katika hili sakata, basi
huyo meneja ni namna moja. Maana hakuwa makini na inawezekana basi hii kazi
kaivamia! Kwa nini hawana mkataba orijino? Hakujua, au hajui maana yake? Kama
hajui kweli, basi hapaswi kuwa meneja na vizuri akifunga mdomo sasa.
Lakini
kwa wale viongozi wa Simba waliomsainisha mkataba Messi, walipaswa kuwa ‘fea’.
Walijua ni kijana mdogo ambaye haelewi mambo mengi ya mikataba au kisheria.
Hivyo walipaswa kumsaidia na kumpa mkataba wake au kumsisitiza awe nao au
kuutunza.
Kweli
mtu anaweza akawa hajui, kwa kuwa walikuwa kati ya makinda wa Simba hata kama
hawakuanza kumkuza tokea akiwa mtoto. Lakini bado walikuwa na jukumu la
kumuelimisha kuhisiana na mikataba na umuhimu wake.
Moja;
walitakiwa kuhakikisha wanampa mkataba wake orijino na pili; walitakiwa
kumsisititia kuhusiaa na mkataba huo kwamba ni lazima autunze kwa ajili ya
baadaye.
Kwa
maana ya nyaraka, klabu ndiyo inaonekana iko vizuri zaidi na Messi ana
upungufu. TFF wanakutana kesho na pande hizo mbili, ukweli utapatikana. Nina
hofu kama Messi ataonekana ameonewa kutokana na upungufu huo.
Hivyo
ni wakati mzuri kwa vijana kujifunza na kuelewa umuhimu wa mikataba hiyo kwa
kuwa mara zote inakuwa na faida wakati husika, kipindi chote cha mkataba na
hata baada ya kwisha kwa mkataba. Hivyo kila anayesaini mkataba, ausome au
asomewe na anayemwamini na kuuelewa. Pia awe na kopi yake orijino. Hayo
yangefuatwa, sasa kusingekuwa na mgogoro huu wa Singano.
Kaka huyo Popu ni tapeli mkubwa na ni hatari sana kwa kuchezea makaratasi
ReplyDeleteWAANDISHI WA HABARI MSIWE NA USHABIKI. LAZIMA TUKUBALI KUWA HUYU DOGO ANAJUA NINI ANACHOKIFANYA, HIYO COPY YA MKATABA AMETENGENEZEWA MTAANI, KWA NINI HANA ORIJINO???
ReplyDeleteKWENYE KUSAINI UNAPEWA ORIJINO, YEYE YA KWAKE IKO WAPI???
KUNA BAADHI YA WATU WAJINGA WANAMVUTA MASIKIO HUYO DOGO NA KWA UJINGA WAKE ANAFIKIRI ANAWEZA AKACHEZA NA AKILI ZA WATU.
YEYE AKUBALI KUWA ALISHAFANYA MAKOSA KUSAINI MKATABA WA MUDA MREFU, ANAPOONA WENZIE ALIOANZA NAO AKINA NDEMLA, NA MKUDE WANAKUNJA MIKWANJA YAO SASA NAYE AKAINGIA TAMAA ILI NAE APATE.
KWA UJUMLA WAANDISHI WENGI WA BONGO HAWAKO FAIR, WAO WANAJADILI AS IF MCHEZAJI KAONEWA TU BILA KUANGALIA UPANDE WA PILI. NA SUALA HILI LIKIENDA POLISI HUYU DOGO ATAFUNGWA MAANA HANA ORIGINAL, NANI ATA-BASE KWENYE COPY....!?