SEITZ (KUSHOTO), MMOJA WA WATAKAOFANYA KAZI NA TOTO KUHAKIKISHA MAMBO YANAKWENDA VIZURI. |
Klabu
ya Toto African ya Mwanza imepata neema baada ya kuingia makubaliano na
wataalamu wa soka kutoka nchini Ujerumani.
Wataalamu hao watafanya kazi pamoja na Toto kuhakikisha inafanya vizuri na ikiwezekana kuwa klabu bora ya nne baada ya Yanga, Simba na Azam.
Kwa
mujibu wa Msemaji wa Toto African, Cathbert Japhet, amesema wataalamu hao
watatoa ushirikiano katika masuala kadhaa ya kiufundi.
“Pamoja
na hivyo tunategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwa Chama cha Soka Mkoa wa
Mwanza na ofisini ya Mkuu wa Mkoa pia.
“Lengo
ni kuifanya Toto African kuwa timu ya Wanamwanza kwa faida ya mkoa kwa ujumla
na kuachana na ushabiki wa timu za Dar es Salaam,” alisema.
Mmoja
wa wataalamu hao kutoka Ujerumani ambao watashiriki katika kusaidia Toto ni
Jurgen Seitz.
Imeelezwa,
Seitz alikuwa nchini Aprili, mwaka huu na alitembelea jijini Mwanza ambao ni
mji dada wenye uhusiano na jiji la Wurzburg wa nchini Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment