Wamiliki na wafanyakazi wa Global
Publishers, leo wameuaga mwili wa Robert Tilya, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni
hiyo.
Robert alikuwa mmoja wa wadau wa
michezo kwa kuwa alizunguka sehemu mbalimbali za michezo akiwa na waandishi wa
gazeti namba moja la michezo nchini la Championi.
Alifariki wiki iliyopita katika ajali
ya gari iliyotokea External jijini Dar es Salaam.
Mwili wake umesafirishwa kwao mkoani
Kilimanjaro kwa mazishi.
Mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu za kaburi.
Ampumzishe kwa amani.







0 COMMENTS:
Post a Comment