June 13, 2015


Mbunge wa Singida Mjini (CCM) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohamed Enterprises ambaye ni mwanachama na shabiki mkubwa wa Simba, Mohammed Dewji, ndiye kinara wa utajiri nchini.

Jarida la Uchumi la Forbes, mapema wiki hii limemtaja Dewji, 40, kwa mara nyingine kuwa tajiri namba moja Tanzania akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.25.

Mfanyabiashara Rostam Aziz, 50, ametajwa kushika namba mbili ya utajiri nchini akiwa na utajiri wa dola bilioni moja. Hata hivyo, Dewji anashika nafasi ya 1500 kwa utajiri duniani huku Rostam akishika nafasi ya 1741.


Bado kwa Afrika, tajiri Aliko Dangote ameendelea kuwa kinara wa utajiri akiwa na utajiri wa dola bilioni 17.8 alizopata kupitia uwekezaji wa kampuni za saruji, sukari na bidhaa za nafaka.

Kupitia kampuni yake ya MeTL, Dewji amewahi kuidhamini Simba na kuisaidia kupata mafanikio makubwa mwaka 2003 ilipofanikiwa kuing'oa Zamalek ya Misri kwenye Klabu Bingwa tena kwa kuivua ubingwa wakati huo ikiwa ndiyo timu bora Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic