Mshambuliaji mpya wa Yanga, Malimi Busungu, sasa anatamba katika mitaa
ya Jiji la Dar es Salaam akiwa na gari lake Toyota IST alilokabidhiwa muda
mfupi tu baada kujiunga na timu hiyo.
Busungu alijiunga na Yanga hivi karibuni kwa dau la usajili la Sh
milioni 25 akitokea Mgambo JKT ya Tanga ambayo aliichezea kwa mafanikio msimu
uliopita.
Busungu amesema anatumia gari
hilo katika mizunguko yake ya kawaida ndani ya Dar es Salaam na anajisikia
furaha kuwa nalo.
“Nashukuru Mungu gari langu nimeshapewa na sasa napiga nalo misele
na ukinikuta kwenye daladala basi nimependa mwenyewe au kuna tatizo, kazi
iliyobaki ni kuthibitisha thamani yangu kwa Yanga,” alisema Busungu.
Straika huyo kwa sasa yupo katika kambi ya kikosi cha mjumuisho
cha Taifa Stars ambacho kimebaki jijini Dar es Salaam kikifanya mazoezi.







0 COMMENTS:
Post a Comment