Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), kimezimwagia sifa timu za vijana za Ilala na Kinondoni zilizoshiriki katika michuano ya kuwania ubingwa wa taifa chini ya miaka 13,ambapo fainali zake zimefanyika jiji Mwanza mwishoni mwa wiki.
| HEKAHEKA KATIKA LANGO LA KINONDONI, BEKI WAKE (MWENYE JEZI YA ZAMBARAU) AKIJITAHIDI KUONDOSHA HATARI. KINO WALISHIKA NAFASI YA TATU KWA KUICHAPA MARA KWA MABAO 2-1 KWA MIKWAJU YA PENALTI. |
Katika michuano hiyo Ilala imetawazwa kuwa mabingwa wapya baada ya kuikandamiza mabao 3-2 timuya Alliance,katika mchezo wa fainali,huku kikosi cha Kinondoni kikimaliza katika nafasi ya tatu.
Matokeo hayo yamepigiwa makofi na uongozi wa DRFA,na kuzitaka timu hizo ziendee kukaza kamba ili kufikia mafanikio yanayohitajika katika medani ya soka
hapa nchini.
Mwenyekiti wa chama hicho, Almas Kasongo, amesema uwezo uliooneshwa na timu hizo zilizopo katika himaya yake kwa muda wote wa mashindano, zinatoa taswira za kuwapata wachezaji wazuri wa baadaye kwenye vilabu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam na kwamba ni dira ya mkoa huo kuwa kitovu cha wachezaji nguli wa wakati ujao.
Aidha Kasongo ameipongeza
Tff kwa kuwepo na mashindano hayo ya ubingwa wa taifa kwa vijana
chini ya miaka 13,na kuwataka wendeleze kwa nguvu zote mipango waliyonayo
yakuibua na kukuza vipaji vya soka kwa vijana.
IMETOLEWA NA DRFA,
Omary Katanga, Mkuu wa Habari na Mawasiliano DRFA
IMETOLEWA NA DRFA,
Omary Katanga, Mkuu wa Habari na Mawasiliano DRFA







0 COMMENTS:
Post a Comment