KASEKE (KUSHOTO) AKIWA TAIFA STARS |
Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Deus Kaseke, aliyetokea timu ya
Mbeya City ya jijini Mbeya, ametangaza vita kwa kiungo mwenzake, Simon Msuva au Haruna Niyonzima,
kwa kusema kuwa atajipanga kuhakikisha anapangwa katika kikosi cha kwanza.
Kaseke amesema ni lazima aonyeshe uwezo wa juu kuliko Simon Msuva
kwa kuwa anataka akiwa Yanga acheze namba 11.
Kaseke amesajiliwa na Yanga hivi karibuni ambapo amekuja kuziba
pengo la Mrisho Ngassa aliyetimkia Afrika Kusini katika timu ya Free State.
Kaseke amesema kuwa kati ya
namba tatu anazocheza 10, 11 na 7, namba 11 pekee ndiyo ambayo anaona
ataitendea haki iwapo kocha Hans Pluijm atampanga.
“Mimi nacheza nafasi tatu ambazo ni saba, 10 na 11, lakini namba
11 kwa upande wangu ndiyo ninaiona kuwa huru zaidi pindi ninapoicheza, hivyo
ningependa kocha anipange namba hiyo na nitajituma kuhakikisha napata nafasi,
najua kuna wengine wanaweza kucheza hapo lakini nikijituma najua nitapewa
kipaumbele.
“Iwapo mwalimu atanipanga katika namba hiyo, nitakuwa vizuri zaidi
kuliko hizi nyingine zilizobakia.
“Kuhusu ushindani wa namba, nimejipanga vyema hata kama kuna watu,
nitajituma kadiri ya uwezo wangu kuweza kumshawishi kocha,” alisema Kaseke.
0 COMMENTS:
Post a Comment