June 19, 2015

Mshambuliaji wa Azam FC, Mcha Hamis, amewekewa bandeji ngumu P.O.P kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kupata majeruhi kwenye goti lake la mguu wa kushoto, hivyo amepewa mwezi mmoja kuwa nje ya uwanja na atakosa mashindano ya Kombe la Kagame.


Kwa mujibu wa Daktari wa Azam, Mbarouk Mlinga ni kuwa, Mcha atakaa kwa kipindi cha mwezi mmoja nje ya uwanja.

“Alivunjika kidogo kwenye goti, ndiyo maana tukamwekea P.O.P ili awe sawa. Atakaa na bandeji hiyo kwa muda wa wiki mbili na tangu alipowekewa hadi leo, ameshamaliza wiki moja, hivyo Alhamisi ijayo atatolewa," alisema Mbarouk.


Alisema wachezaji wengine ambao wana programu maalum ni beki wa kushoto, Waziri Salum aliyeumia unyayo, beki wa kati, Abdallah Kheri aliyechanika nyama ya paja na mshambuliaji Joseph Kimwaga aliyefanyiwa upasuaji Afrika Kusini lakini Farid Mussa aliyekuwa anasumbuliwa na nyama za paja amepona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic