Kufuatia ukakasi wa tuzo za Ligi Kuu ya Bara zilizotolewa
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), shirikisho hilo limeibuka na kusema kuwa
Bodi ya Ligi haijakurupuka kufanya maamuzi hayo.
Kauli hiyo imetolewa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wadau ambao
wameonyesha kutoridhishwa na tuzo ya kipa bora ambaye ni Shaban Kado pamoja na
kocha bora, Mbwana Makata.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema anashindwa kuelewa ni kwa
nini watu wanazibeza tuzo hizo ambazo zimetolewa na watu wenye akili zao na wao
kama TFF wamekubaliana nazo.
“Watu wanashindwa kuelewa kwani sisi kama viongozi tunaamini kabisa
maamuzi yaliyofanywa na Bodi ya Ligi pamoja na kamati ya mashindano ni ya haki
wala hawajakurupuka.
“Ieleweke kuwa katika maisha binadamu huwa hawaridhiki na hawakosi
cha kusema ila kama wanaona kuna upungufu wahakikishe wanatoa maoni yao kwa
ushahidi ili msimu ujao yafanyiwe kazi ila kwa msimu huu hakuna anayeweza
kubadili maamuzi ambayo yameshafanywa,” alisema Mwesigwa.
Nilifikiri watakuja na vigezo vilivyotumika kuwapata au kuwapa hao.. Ila ni blah blah as usual
ReplyDelete