June 26, 2015


Mshambuliaji mkongwe Mussa Hassan Mgosi, jana alianza rasmi mazoezi na klabu yake mpya ya Simba kwa mkwara mzito ambapo amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kusubiri mambo mazuri kwa kuwaambia kuwa amerejea Msimbazi kwa kazi na siyo maneno.


Mgosi aliyerejea SImba akitokea Mtibwa Sugar alikuwa injini na kuwaongoza wachezaji chipukizi kwenye kila programu katika mazoezi hayo yanayoendelea kwenye Gym ya Chang’ombe tangu Jumanne wiki hii yakisimamiwa na kocha msaidizi, Selemani Matola.


Kuanza mazoezi katika siku ya kwanza tu imeonyesha kuwa kweli Mgosi ni mmoja ya wachezaji wakomavu na wanaoyajua majukumu yao.

Kwani idadi ya walioanza mazoezi ni wachache sana ikionyesha wengi wataingia mazoezini baada ya siku mbili tatu au nne.


Lakini mkongwe huyo amekuwa kati ya wale walioanza mazoezi mapema jambo ambalo wengine wanapaswa kujifunza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic