June 26, 2015


Siyo mara ya kwanza kutokea lakini hii ya safari hii inaweza kuwa ni jibu. Unakumbuka mapema mwaka huu mashabiki wa Simba walilisukuma gari la Emmanuel Okwi mara baada ya timu hiyo kupata ushindi dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam? Sasa straika wa Yanga amejibu.


Jibu hilo limetoka kwa Mrundi, Amissi Tambwe ambaye mashabiki waliamua kusukuma gari lake aina ya Toyota Brevis kutokana na kufurahishwa na uwezo wake katika mechi dhidi ya Friends Rangers.


Tukio hilo lilitokea kwenye Uwanja wa Karume mara baada ya mechi hiyo ya kirafiki ambapo kundi kubwa la mashabiki wa Yanga liliisukuma gari kutoka ndani ya uwanja mpaka nje huku likimshangilia kwa kuimba “Tambwe, Tambweee, Tambweeeee!”



Mashabiki wengine walikuwa wakisafisha vioo vya gari hilo huku Tambwe akiwapungia mkono.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic