June 26, 2015

MWALYANZI...
Mambo yanakwenda yanabadilika, sasa si kama zamani! Zikiwa zimepita siku mbili tu tangu kuonja mazoezi na timu yake mpya ya Simba, kiungo wa timu hiyo, Peter Mwalyanzi, juzi Jumatano aliivamia Yanga kwenye mazoezi.


Kiungo huyo aliyetokea Mbeya City, aliifuata Yanga wakati timu hiyo ikiwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume, mchezo ambao ulichukuliwa kama mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.

Simba na Yanga ni timu pinzani zaidi Tanzania na mara nyingi wachezaji wake wamekuwa wagumu kuchanganyika pamoja katika ishu mbalimbali zinazohusiana na mambo ya soka.
 
KASEKE (KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI...
Mwalyanzi alifika mazoezini hapo kwa lengo la kumuangalia ‘mshkaji’ wake Deus Kaseke ambaye walikuwa wakikipiga pamoja Mbeya City msimu uliopita lakini kwa sasa ni mali ya Yanga.

Mwalyanzi alipoulizwa sababu za kufika uwanjani hapo alicheka tu na kutotaka kufafanua zaidi.


Mbali na Mwalyanzi, pia kulikuwa na wadau mbalimbali wa Simba katika mchezo huo, akiwemo makamu wa rais wa timu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na kinda wa timu hiyo, Issa Abdallah.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic