Wakati Tanzania
imepoteza mechi yake ya kwanza katika kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika,
timu zote za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, zimefanya vizuri.
Rwanda ikiwa
ugenini chini ya nahodha Haruna Niyonzima imeshinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi
ya Msumbuji.
Bao hilo moja
limeifanya limeiweka Rwanda katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri zaidi kuwania
kucheza Afcon.
Timu nyingine
imefanya vizuri Ethiopia imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho. Kenya nayo
ikatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Congo.
Sudan ikiwa
nyumbani, imeitwanga Sierra Leone kwa bao 1-0 ikiwa jijini Kharthoum huku DR
Congo ikiibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Madagascar.








0 COMMENTS:
Post a Comment