June 14, 2015


Taifa Stars imeanza vibaya kampeni ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0.


Katika mechi iliyochezwa jijini Alexandria, Stars imefungwa mabao hayo na wenyeji wake Misri ndani ya dakika 45. Mabao matatu ya Misri yamefungwa na wachezaji wake nyota akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Mohammed Salah.
SALAH

Hadi mapumziko timu hizo zilikwenda zikiwa hazijafungana lakini kipindi cha pili kikaonekana kuwa cha mateso kwa Stars.

Misri ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 61 kupitia kwa Rami Rabia kabla ya Basemi Morsi kufunga la pili katika dakika ya 65.

Salah ndiye aliyeikata maini Stars baada ya kufunga bao la tatu katika dakika ya 70. Bao hilo lilionyesha kuimaliza kabisa Stars iliyoweka kambi nchini Ethiopia kabla ya kwenda nchini Misri kwa ajili ya pambano hilo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic