June 27, 2015


Simba wanasubiri ujio wa straika Laudit Mavugo lakini Rais wa Vital’O ya Burundi anayochezea mchezaji huyo, Bikolimana Benjamin, amesema: “Mnajidanganya, Mavugo haji Tanzania wala Simba.”

Uongozi wa Simba na mashabiki wao kwa hamu kubwa wanamsubiri Mavugo aje nchini wikiendi na kuanza mazoezi keshokutwa Jumatatu lakini huenda asije tena nchini.

Rais wa Vital’O, Bikolimana amezungumza na SALEHJEMBE na kusema,  Mavugo hawezi kuja Tanzania mpaka watakapomalizana na Simba.

Alisema tangu Simba walipofika nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo ya kunasa mchezaji huyo na kushindwa kufikia makubaliano, hawakurudi tena kwa ajili ya kumalizana na klabu hiyo.

“Sisi tupo tayari kumwachia Mavugo ajiunge na Simba kwa sababu tuna uhusiano nao mzuri ila tutafanya hivyo baada ya kuwa tumemalizana nao.

“Kuna mambo ambayo katika mazungumzo yetu ya awali yaliyofanyika hapa Burundi, tulikubaliana nao na tukawaambia kuwa wakiyatekereza tutawaachia Mavugo, hata hivyo tangu walipoondoka wamekaa kimya,” alisema Benjamin.

Alisema endapo Simba wataendelea kukaa kimya, basi wapo tayari kumuuza mchezaji huyo sehemu nyingine, kwani tayari kuna timu kutoka Ivory Coast inamhitaji.

Simba ilitangaza kumsainisha mkataba Mavugo, lakini Benjamin alipoulizwa kuhusu hilo aling’aka: “Nini? Wamemsainisha? Watakuwa wamejifurahisha kwani Mavugo bado ana mkataba na sisi na walichofanya hatukitambui, wanatakiwa kumalizana na sisi kwanza.”

Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema: “Hakuna tatizo, tunashughulikia jambo hilo na hapa nipo kikaoni.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic