Kazi ya ukocha ni pasua kichwa, tena inaumiza na
kutesa kweli kutokana na presha kubwa. Hata hivyo, ina raha yake.
Kocha wa zamani wa QPR ambaye aliachia ngazi
wiki chache kabla haijaporomoja daraja, amenunua bonge la jumba lenye thamani
ya pauni milioni 4.
Harry Redknapp amenunua jumba hilo katika eneo
la Poole Dorset nchini England na sasa anaishi hapo.
Kocha huyo mkongwe mwenye miaka 68 anaishi
katika jumba hilo lenye vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea pamoja na
lifti.
Jumba hilo lina lifti kwa kuwa kocha huyo
alifanyiwa upasuaji wa magoti yote na alitangaza kuacha kazi ili afanyiwe
upasuaji.
DAILY MAIL.
0 COMMENTS:
Post a Comment