Swansea City imefanikiwa
kumnasa kiungo mshambuliaji wa Ghana, Andre Ayew.
Ayew ambaye ni mtoto mwa
gwiji wa Ghana, Abeid Ayew amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Swansea
inayoshiriki Ligi Kuu England.
Swansea imeishinda West
Ham United iliyokuwa inamuwania pia na kumnasa kiungo huyo mwenye miama 25.
Ayew ameondoka Marseille
baada ya mkataba wake kwisha, hivyo ametua Swansea akiwa na faida mkononi.
0 COMMENTS:
Post a Comment