June 3, 2015



Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.


Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:

1. Leodeger Tenga- (Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Vyama Wanachama).

2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)

3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).

4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)

5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)

6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)

7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
TFF.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic