Uongozi wa Yanga imetangaza kuwa, kamwe haitamsajili profesheno
yeyote aliyewahi au anaiyechezea timu za Ligi Kuu Bara na kwamba ni upuuzi
mkubwa kuhusishwa na suala la kumrejesha Emmanuel Okwi kutoka Simba.
Hiyo ni siku chache tangu ivumishwe kuwa Okwi amesajiliwa Yanga
kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.
Ukiachana na Okwi, baadhi ya wachezaji wa kimataifa wanaotajwa kwenye
usajili wa timu hiyo ni Waivory Coast, Pascal Wawa na Kipre Tchetche.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alisema kuwa ili
kuepukana na matatizo, wameona wachukue maamuzi hayo ya kutosajili wachezaji wa
kimataifa wanaozichezea au waliowahi kuzichezea klabu za hapa nchini.
Tiboroha alisema wanaamini wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa
wa kuichezea Yanga ambao wamepanga kuwaleta kutoka Nigeria, Ghana, Zimbabwe na
Sierra Leone ambao wakati wowote watatua nchini.
“Kamwe hautakuja kusikia
Yanga imemsajili mchezaji wa kimataifa aliyewahi au anayeichezea klabu yoyote
inayoshiriki ligi kuu nchini hapa.
“Kama wachezaji wapo wengi tu kutoka kwenye mataifa mbalimbali,
ndiyo maana tumepanga kuwaleta Waghana, Mzimbabwe, Mnigeria na Msierra Leone
ambao watakuja kwa ajili ya kuichezea Yanga.
“Hiyo ni moja ya mikakati tuliyoipanga Yanga katika usajili wetu
wa msimu huu na miaka ijayo, labda uongozi mpya uingie, lakini siyo huu wetu,” alisema
Tiboroha.







0 COMMENTS:
Post a Comment