Mmoja wa makocha
wanaoaminika kuwa ni wakali na hawataki mchezo kazini ni Jose Mourinho.
Kocha huyo wa
Chelsea amefanya kazi katika nchi za Ureno, England, Italia na Hispania na kote
amechukua ubingwa wa nchi.
England amebeba
mara mbili, lakini pamoja na ukali wake, bado anaonekana ni mtu anayejua ‘kucheza’
na akili za wachezaji wake.
Angalia
alivyotengeneza mchezo kama vile wanaoendesha ndege, unaweza ukadhani watoto
wanacheza. Walipojisahau, wakamwagiwa barafu ingawa nahodha John Terry anajua
michezo ya Mourinho, hivyo alikuwa wa kwanza kutimua mbio.
Mfano kuandaa
michezo mbalimbali inayowafanya wacheke sana na kusahau ugumu wa mazoezi au
ukali wake.
Michezo hiyo
inawafanya wajione ni sehemu ya familia na watu wanaotaka kutimiza lengo moja
kwa pamoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment