Washambuliaji wawili wakongwe,
Hamis Kiiza na Mussa Hassan Mgosi wameonyesha ukubwa dawa baada ya kuingoza
Simba kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar kwenye Uwanja wa
Amaan mjini Zanzibar, leo.
Mechi hiyo ni ya kwanza kwa Simba
ambayo imecheza chini ya Kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza aliyejiunga na
Simba kuchukua nafasi ya Goran Kopunovic raia wa Serbia.
Licha ya mechi kuwa kali, Simba
ilicheza taratibu katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Kerr alibadilisha
karibu timu yote na baada ya hapo Simba ilicheza kwa kasi na kuwafanya mashabikiw ake waliokuwa uwanjani hapo
kushangilia kwa nguvu.
Ushindi huo unaifanya Simba kuanza
vizuri kwa maana ya mechi za kirafiki kwa kuwa imekuwa ikiweka kambi tu za
mazoezi kuanzia Lushoto mkoani Tanga kabla ya kutua Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment