| KMKM Baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Gor Mahia, KMKM wanaamini bado wana nafasi ya kufuzu kwenye hatua ya mtoano. |
KMKM
ilichapwa kwa mabao 3-1 na Gor Mahia ya Kenya ambayo imejihakikishia robo
faibnali ya michuano ya Kagame baada ya kushinda mechi ya pili mfululizo.
Kocha
Mkuu wa KMKM, Ali Bushir ‘Shilton’ amesema ana imani kubwa na kikosi chake.
“Kuna
makosa ambayo tunajifunza, soka ndiyo iko hivyo kuna siku mnafanya vizuri na
nyingine mnateleza.
“Uliona
tulivyocheza vizuri hasa kipindi cha kwanza, lakini dakika za mwisho
tukateleza.
“Imani
yangu kubwa tutajirekebisha na kufanya vizuri mechi zilizobaki,” alisema
Bushiri.
KMKM
ina mechi mbili na pointi tatu kibindoni baada ya kuanza michuano hiyo kwa
ushindi halafu ikapoteza mechi ya pili.







0 COMMENTS:
Post a Comment