July 27, 2015


Bobbi Kristina Brown amefariki dunia ikiwa ni miezi sita baada ya kukutwa akiwa bafuni ameanguka.

Msichana huyo mwenye miaka 22, mtoto wa nyota wa muziki Marekani, Bobby Brown aliyezaa marehemu whitney Houston, amekuwa katika hali ya kutojitambua tokea Januari 31, mwaka huu.

Baada ya kukutwa ameanguka bafuni na hajitambui akiwa nyumbani kwake Roswell, Georgia nchini Marekani, alikimbizjwa katika hospitali ya Peachtree Christian Hospice, ambako ndiko mauti yamemkuta jana usiku.

Mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka 48, yeye bafuni katika hoteli moja mjini Beverly Hills.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic